Wamekula ya Mbuzi ...Wanaota Mapembe

Migogoro mingi katika bara la Afrika hutokea kwa sababu ya Madaraka, Viongozi wengi wanapotaka kuingia madarakani hutoa ahadi zenye kuvutia kwa wananchi wao lakini mara wanapoingia madarakani utamu wa madaraka huwazidi na kujikuta wakijaribu kadri wawezavyo kubadilisha Katiba ili waendelee kuongoza. Hali ambayo huzusha migogoro. Ama kweli "Wamekula ya Mbuzi sasa Wanaota Mapembe".

Sunday, May 28, 2006

Ufukala umetukuta!

Nahisi hali inavyokwenda sio nzuri, kwa mtanzania wa kawaida kuweza kuhimili maisha ambayo yanazidi kuwa magumu zaidi kila kunapokucha.

Hebu fikiria pamoja na ugumu wa maisha uliopo sasa unaotokana na ukame na upungufu wa chakula ulioikumba nchi yetu na baadhi ya nchi jirani, limejitokeza tatizo lingine ambalo ni sawa na kupigilia msumari ndani ya kidonda!, tatizo hilo ni kupanda kwa bei ya mafuta.

Bei hiyo imekuwa ikipanda kila kunapokucha na kufikia kipindi ambacho mwananchi wa kawaida kushindwa hata kulipia nauli ya Daladala kwa sababu ya nauli kupanda mara kwa mara.

Kwa hali hii mtanzania hatakuwa na maisha bora hata siku moja kwani Njaa+ bei kubwa ya mafuta = Ufukara uliokithiri.

2 Comments:

  • At 5:42 PM EAT, Blogger charahani said…

    Ndugu yangu Kazonta kweli inaonekana huu ufukara umekusikitisha kiasi kwamba umekosea hata kuandika umeandika 'ufukala' (joke) usijali. Unachokisema ni kweli hali ya Mtanzania ni mbaya kupita kiasi sijui tunakwenda wapi nimetoka huko Shinyanga kwa hakika muda si mrefu tutakuwa na omba omba kibao kupanda kwa bei ya mafuta + ukame+ mgawo+ mengi tu = balaa.

     
  • At 1:35 PM EAT, Blogger Rashid Mkwinda said…

    Naona Charahani anataka kunichekesha kidogo unajua, kuna baadhi ya watu wameathiriwa na 'RA'na wengine wameathiriwa na 'LA' halikadhalika wengine wameathiriwa na ZA,DHA,GA, GHA, MTU, NTU nakadhalika kulingana na lahaja za sehemu watokeako sisi wana fasihi wa Kiswahili tunajitahidi kuwarekebisha na kumjulisha mzee wa kifimbo cheza awacharaze viboko(jokes).

    Okay nikirejea katika mada ni kweli huu UFUKARA ambao unatukumba sisi MAFAKIRI hauna hatima nzuri kwani kinachojadiliwa na hao tuliowapigia kura huku wakitembelea mashangingi na kudai posho isiyomithilika hakinamaana yoyote ikiwa hadi sasa bado mafuta hayajashuka pamoja na kutangazwa kushuka kwa bei.

     

Post a Comment

<< Home