"Kupanga ni Kuchagua"

Kila mwanadamu ana mamlaka ya kubadilisha maisha yake kwa kutumia mazingira aliyo nayo! Mipango mibovu ya maisha yake husababisha maisha yake kuwa mabovu na Mipango bora ya maisha yake husababisha maisha yake kuwa Bora. Hivyo basi chagua maisha yako unataka yaweje?

Wednesday, April 06, 2005

Professa Mark Mwandosya arudisha fomu.

WAZIRI wa mawasiliano na uchukuzi Pro. Mark Mwandosya amerudisha fomu hivi karibuni ya kuomba baraka za kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kusema kuwa anaomba baraka za kugombea Utumishi wa nchi na si utawala wa nchi.

Pro. Mawandosya ambaye alikabidhi fomu za wadhamini 250 wa mikoa 10 miwili ikiwa ya Tanzania visiwani, kwa Katibu wa mipango wa CCM taifa Bw. Jackson Msome ambaye alipokea fomu hizo kwa niaba ya katibu Mkkuu wa CCM taifa Bw. Philip Mangula katika ofisi ya makao makuu ya chama hicho mjini hapa.

Mwandosya ambaye alikuwa ameongozana na mkewe Bibi Lucy Mwadosya, mwanaye wa kwanza Max Mwandosya, Mchumi msaidizi wake Bw. Filbert Meena na msaidizi wake wa karibu Bw. Peter Katto.

Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhi fomu hizo Pro. Mwandosya alisema kuwa yeye hagombei nafasi ya juu ya utawala bali anagombea nafasi ya juu ya utumishi kwa kuwa hapa nchini hakuna mtawala binafsi zaidi ya chama ambacho ni CCM.

“Nagombea nafasi ya juu ya utumishi na si nafasi ya utawala kwa kuwa najua nchi hii inamtawa mmoja tu ambaye ni CCM ambaye atatawala miaka nenda rudi lakini si mtu binafsi ndiyo mtawala” alisisitiza.

Alisema kuwa mpaka sasa kuna baadhi ya wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea urais tayari wamekanza kujiita wagombea na kusahau kabisa kuwa wao si wagombea nafasi hiyo ya utumishi.

“Hapa katika fomu zangu pameandikwa saini ya muombaji na wala hapajaandikwa saini ya mgombea urais sasa tunasahau kuwa sisi bado si wagombea urais ila waombaji wa kuteuliwa kuwa wagombea nafasi hii”

Alisisitiza kuwa katika siasa ndani ya chama hakuna mtu mwanasiasa maarufu pekee bila chama na kuongeza kuwa hakuna muombaji wa kuteuliwa kuwa mgombea nafasi hiyo maarufu ambaye si mwana CCM.


Aidha Pro. Mwandosya alisema kuwa katika uchaguzi huu hakuna mtu ambaye atashinda wala kushindwa zaidi ya chama husika kushinda au kushindwa na si mtu binafsi.

“Hapa napenda nikukumbusheni ndugu zangu kuwa tusijisahau na kufikiria kuwa kama ukishindwa katika uchaguzi mkuu huu utakuwa ni wewe hapa takayeshindwa au kushindwa kitakuwa ni chama husika na si mtu binafsi”

aidha Pro. Mwandosya aliwakumbusha baadhi ya wanoomba baraka hizo kuwa wasijisahau na kuona kupendwa ndio kigezo kikubwa cha kuteuliwa kuwa mgombea wa urais katika awamu ya nne.

Alisema kuwa kuna baadhi ya wagombea ambao walijiwekea taratibu zao wakati wa kutafuta wadhamini jambo ambalo lilileta, hamasa, vitimbi na vurugu nakuongeza kuwa hizo ni tabia za baadhi ya wanadamu ambao hupenda kujionyesha kuwa wanapendwa.

“Napenda tu kuwaambia wana CCM kuwa hali hii ni sawa na tishio kwa wanaofanya maamuzi kuwa msiponichagua ni mizengwe”

Aidha aliwahukuru wana ccm wote ambao walijitokeza kumdhamini na wal;e ambao hawakupata nafasi hiyo ya kumdhamini na kuongeza kuwa iwapo ataipata nafasi hiyo ya utumishi basi atawatumikia kwa moyo wake wote.

“Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaahidi kama nitaipata nafasi hiyo basi nitawatumikia kwa moyo wangu wote , kwa nia yangu yote na kwa akili zangu zote” alisisitiza.

mwisho

0 Comments:

Post a Comment

<< Home