"Kupanga ni Kuchagua"

Kila mwanadamu ana mamlaka ya kubadilisha maisha yake kwa kutumia mazingira aliyo nayo! Mipango mibovu ya maisha yake husababisha maisha yake kuwa mabovu na Mipango bora ya maisha yake husababisha maisha yake kuwa Bora. Hivyo basi chagua maisha yako unataka yaweje?

Saturday, April 16, 2005

Hivi ni kweli Dodoma haina uwezo wa kuwa na Chuo Kikuu?

Dodoma ni makao makuu ya nchi ya Tanzania na inapatikana katikati ya nchi ikiwa na wakazi takribani zaidi ya million moja ambao wanatoka katika makabila mbalimbali.

Kwa ujumla Dodoma ni mkoa ambao wakazi wake wakuu ni kabila la Wagogo ambao ni karibu zaidi ya nusus ya wakazi wa hapa wakifuatiwana kabila la Warangi ambao wao hupatikana zaidi katika wilaya ya Kondoa.

Kama mikoa mingine wakazi wa Dodoma hujishughulisha na shughuli za kilimo ikiwemo kilimo cha mtama, mahindi, Karanga pia hujishughulisha zaidi na ufugaji wa wanyama kama ng'ombe mbuzi na kondoo.

Pamoja na hayo Dodoma ni makao makuu ya nchi yetu ambayo mkoa huu ulipewa hadhi hiyo toka enzi za mwalimu Nyerere.

pamoja na kupewa hadhi ya kuwa makao Makuu ya nchi mkoa huu bado uko nyuma zaidi katika maswala ya kielimu, hii ni kutokana na kutokuwa na taasisi yoyote inayotoa elimu ya juu.

Hii kwa njia moja ama nyingine imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya Mkoa huu kwa njia moja ama nyingine kwani tunakubaliana kuwa bila elimu mwanadamu hata pata maendeleo thabiti.

Ni kutokana na hili basi imenibidi kujiuliza ni kwa nini mkoa huu ukakosa taasisi inayotoa elimu ya juu katika kipindi chote hicho toka utangazwe kuwa makao makuu ya nchi.

Hili ni swali ambalo kwa siku nynigi limekuwa likiniumiza kichwa pasipo kulipatia majibu sahihi, kuhusu mustakabali mzima wa elimu mkoani hapa.

Tukumbuke kuwa hapo awali mkoa wa Dodoma ulikuwa na tatizo kubwa sana la maji ambalo kwa sasa halipo tena.

Hali hii ilisababisha wananchi wengi wa Mkoani hapa kupata ugonjwa wa Trachoma ambao ulishambululia sana macho na kusababisha wananchi wengi kupata upofu.

hivyo basi kama tatizo la mzji halipo tena kwanini Mkoa bado unakosa chuo kikuu hata kimoja?

NAOMBA MCHANGO WAKO KUHUSU MADA HII KOKOTE ULIKO BAADA YA HAPO NITAIMALIZIA .......!

1 Comments:

  • At 6:51 AM GMT+3, Blogger Paula said…

    Hudson,
    I think that is a positively wonderful idea. I wish I could read yours too. I don't know anyone from Africa, I think it would be very interesting to get to know one another!

     

Post a Comment

<< Home