Hivi kwa hali hii tutapata maendeleo?
Pamoja na kuwa Tanzania ni masikini sana, nchi hii imebarikiwa kwa kuwa na aina mbalimbali za madini katika ardhi yake.
Madini haya yametanda karibu kila kona ya nchi hii ukianzia pembe ya kusini hadi kasikazini mwa nchi, na kwa bahati kubwa ni nchi pekee ambayo imebahatika kuwa na madini ya Tanzanite.
Madini haya ni madini pekee ambayo yanapatikana katika Tanzania tu, na ni Madini yenye thamani kubwa zaidi.
Pamoja na kuwa na utajiri mkubwa wa madini na vitutio mbalimbali kama mlima Kilimanjaro, Mbuga mbalimbali za Wanyama, wananchi wake bado wako katika wimbi kubwa la umasikini.
Umasikini huuumekuwa ukiongezeka kila kunapokucha na kufanya hali za wananchi hata kumudu chakula cha kila siku kuwa ni matatizo na kufanya baadhi ya watu kutokufikisha milo miwili kwa siku.
Lanini basi ni kwanini wananchi wa Tanznia wanazidi kuwa masikini wakati kuna maliasili za kutosha katika maeneo yao?.
Hili ni swali ambalo mimi hujiuliza mara kwa mara na kukosa jibu la uhakika kwani hakuna sababu ambayo inaweza kutolewa kwa watu ikakubalika kama si makosa ya Serikali kutokuweka sera sahihi juu ya wananchi wake na wageni ambao sisi huwaita kama wawekezaji.
Serikali kwa hili inapaswa kuwajibika kwani imekuwa ikiangalia na kukaa kimya bila kuweka mikakati sahihi ya kuwalinda wazawa wa Taifa hili.
Hili linazidi kujidhihirisha hasa baada ya wawekezaji kuja na kuwekeza kwenye sekta ya madini ambao wamesababisha migogoro mbalimbali kati yao na wachimbaji wadogo wadogo wa madini.
Serikali badala ya kuweka mazingira mazuri na kuhakikisha inaweka mikakati sahihi ya kuwalinda wananchi wake ambao ni masikini, imekuwa ikiwakumbatia zaidi wageni na kusababisha wananchi hawa kutumia nguvu katika kudai maeneo yao.
Ni nani ambaye hajawahi kusikia migogoro ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite na wamiliki wa ardhi wa kigeni huko Mirelani?, ni kweli kuwa migogoro hii ipo na muwajibikaji ni serikali kwa kutowatengea wachimbaji hawa maeneo maalum.
Pia jambo jingine imekuwa ni kawaida kwa wachimbaji madini kutoka nje ya nchi kuja kuchimba madini na kuchukua hata ile michanga ya madini.
Sasa hebu fikiria kuwa kama hata tu ule mchanga unachimbuliwa na kupelekwa nje ya nchi kwa kisingizio eti kuwa hapa hakuna kiwanda ambacho kinaweza kufanya usafishaji wa madini hayo, hatuoni kuwa tunakuza soko la ajira kwa wenzetu Ulaya?.
Wakati sasa umefika kwa serikali kuweka mikakati sahihi ya kuhakikisha kuwa wawekezaji wanapokuja hapa nchini wanapewa mazingira ambayo yatawalazimu kujenga viwanda hapa nchini ili kukuza soko la ndani la ajira kwa wananchi wa Tanzania.
Mwisho.
0 Comments:
Post a Comment
<< Home