"Kupanga ni Kuchagua"

Kila mwanadamu ana mamlaka ya kubadilisha maisha yake kwa kutumia mazingira aliyo nayo! Mipango mibovu ya maisha yake husababisha maisha yake kuwa mabovu na Mipango bora ya maisha yake husababisha maisha yake kuwa Bora. Hivyo basi chagua maisha yako unataka yaweje?

Thursday, May 12, 2005

Mke wa Rais wa Kenya aingia studio na kuleta fujo.

Kama katika historia ya wanawake na wake wa viongozi wa nchi mama Lucy Kibaki atakumbukwa zaidi na wanahabari hasa baada ya kuwa na hali ya kutokuelewana baina ya mama Lucy Kibaki Mke wa Rais wa Kenya Mwai Kibaki na Vyombo vya Habari.

Kutokuelewana huko kwa kweli kumefikia hatua mbaya hali ambayo ilifika kipindi mama huyo akamuwasha vibao mpiga picha mmoja wa TV mjini Nairobi.

Hali hii imewashitua wanahabari wengi ulimwenguni na mimi nikiwa miongoni mwa jamii ya wanahabari nimeamua kuwawekea habari hii ili na nyinyi muweze kusoma.

Ili kupata habari kamili bonyeza hapa.

0 Comments:

Post a Comment

<< Home