"Kupanga ni Kuchagua"

Kila mwanadamu ana mamlaka ya kubadilisha maisha yake kwa kutumia mazingira aliyo nayo! Mipango mibovu ya maisha yake husababisha maisha yake kuwa mabovu na Mipango bora ya maisha yake husababisha maisha yake kuwa Bora. Hivyo basi chagua maisha yako unataka yaweje?

Thursday, June 30, 2005

HUU UKOMAVU WA KIUONGOZI



Katika nchi zetu nyingi za Kiafrika ni vigumu sana na ninaweza kusema kuwa hiwezekani kwa mataifa mengine isipokuwa tu kwa Rais aliyeonekana kuwa amekomaa kimsimamo na anaye lilia haki ya wananchi wake Huyu si mwingine ni Raisi wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki.

Mheshimiwa huyu pasipo lawama wala papara amemfukuza kazi Makamu wake wa Rais ndugu Jacob Zuma kwa kuhusishwa na ulaji wa rushwa katika uongozi wake.kitendo hiki si kigumu tu kwa mfukuzaji bali hata kwa wananchi wenyewe kukubaliana nacho kwani tumesha sikia kuwa baadhi ya vyombo vya habari vikitangaza kuwa Wapambe wake ambao ni miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo wakipinga kufukuzwa kwake.

Hiki ndicho kilichonifanya hata mimi kukumbuka ile kashifa ya sukari ambayo iliishia kwa mhusika kuambiwa kuwa ajiuzuru kwa manufaa ya umma, kwa kweli uamuzi kama huu kwa nchi yetu bado ni kitendawili kwani yanafanbyika hata yaliyomakubwa zaidi ya hili la mheshimiwa Zuma lakini wahusika huambiwa wajiuzuru kwa maslahi ya Taifa.

Hivi hii ni kwa maslahi ya Taifa au yake Binafsi?, kwani yeye akijiuzuru taifa litafaidika vipi? zaidi ya kumwacha yeye akitumia tu yale mavumba ambayo ameyapata kutokana na ukiukaji wa sheria alioufanya? kwa nini aifukuzwe na kupelekwa mahakamani kama huyu Mh. Zuma?

Kwa kweli inawezekana kwa kiongozi kufanya kosa na kufukuzwa kama alivyofanya mwenzetu wa huko Afrika ya Kusini na kupelekwa mahakani, bali kinachofanya jambo hili lishindikane ni kulindana kwa baadhi ya viongozi ambao wanakuwa madarakani na kushindwa kutumia dhamana yao waliopewa na wananchi.