"Kupanga ni Kuchagua"

Kila mwanadamu ana mamlaka ya kubadilisha maisha yake kwa kutumia mazingira aliyo nayo! Mipango mibovu ya maisha yake husababisha maisha yake kuwa mabovu na Mipango bora ya maisha yake husababisha maisha yake kuwa Bora. Hivyo basi chagua maisha yako unataka yaweje?

Friday, July 15, 2005

Mpwapwa wapata Askofu Mpya


Kanisa la Anglican Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa limemchagua askofu mwandamizi mpya atakaye chukuwa nafasi ya Askofu wa sasa atakapomaliza muda wake hapo mwaka 2007.

Kwa mujibu wa Tarifa iliyotolewa na Kanisa hilo na Kutiwa saini na Katibu mkuu wake Dr.Akili Mwita jana ilisema kuwa Askofu huyo atachukuwa atachukuwa rasmi kiti cha uaskofu hapo mwaka 2007 baada ya skofu wa sasa kustaafu.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Mchungaji Canoni Jacob Erasto Chimeledya (48) alichaguliwa tarehe 12/7/2005 na sinodi maalumu ya uchaguzi katika Kanisa Kuu la watakatifu wote mjini Mpwapwa, uchaguzi ambao pia ulihudhuriwa na katibu mkuu wa Kanisa Anglican Tanzania.

Uchaguzi huo ambao ulihudhuriwa na wajumbe wapatao 230 ulisimamiwa na Askofu wa Dudley Mageni wa D ayosisi ya morogoro na Askofu huo atachukuwa nafasi ya Askofu wa sasa Dr. Simoni Chimwanga.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Ibada ya kumweka wakfu kuwa Askofu itafanyika Jumapili ya Tarehe 9/10/2005 ambayo itaongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu Donald Mtetemela wa Kanisa Anglican Tanzania.

Canon Chimeledya alizaliwa huko Zoisa katika wilaya ya Kongwa 1958 na kupata Elimu ya Shahada ya Theolojia katika chuo Cha Paulo Mtakatifu huko Limuru nchini Kenya na baadae kupata Shahada ya Uzamili wa Theolojia katika chuo cha Virginia huko Marekani mwaka 2003.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Canon Chimeledya ameshawahi kufanya kazi mbalimbali, kuwa kasisi wa mitaa na kwa sasa ni Mkuu wa Chuo cha Theolojia cha Mt. Filipo cha Kongwa, pia ameoa na ana watoto wanne.

1 Comments:

  • At 10:37 PM GMT+3, Blogger Jeff Msangi said…

    Ahsante kwa taarifa hii.Naomba unisaidie jambo moja.Ningependa sana kujua huyu jamaa anasemaje kuhusu ushoga na kanisa la Anglican huku kuruhusu mahusiano kama hayo?Kazi njema.

     

Post a Comment

<< Home