Azimio la Dodoma, ndio msimamo wetu!

Hivi karibuni kilifanyika kikao cha wanamtandao wa magazeti tando, katika kikao hicho kilichofanyika mjini Dodoma kilipitia na kuweka taratibu mbalimbali ambazo zinashauriwa kufuatwa na wanamtandao popote pale Duniani.
Soma hapa maazimio ya kikao hicho.
Katika picha hapo juu, kutoka kushoto ni Regnard Simoni, Hudson Kazonta, Martha Beatrice Mtangoo na Kipande ya jitu Mr. Mark Msaki, ambapo baada ya kikao wanamtandao walikuwa wakijadiliana baadhi ya mambo kwenye Kompyuta. (Picha kwa hisani ya Ibrahim Joseph)



6 Comments:
At 7:04 PM EAT,
Boniphace Makene said…
yaani huko Dodoma mnatamba sana na kubadili mahekalu yenu. Ngoja tu na mimi nawasoma soma, lakini pongezi sana washkaji kwa kazi ya kuunda azimio. Hili litabaki katika historia ya maisha yenu. Wengi tulkibaki na mawazo lakini ninyi mmepiga hatua. Mmegusa kabisa mazungumzo yangu ya jana na Mwaipopo na kila jambo mmeweza kuliweka bayana. Haya hamjanambia nani aliongoza kikao. Katibu na nini yafuatayo.
At 9:38 PM EAT,
Bwaya said…
Kaka asante sana kwa kunitembelea. Nimepitia pitia nyumbani kwako, nataraji kurudi tena baadaye kidogo. Kazi nzuri.
At 11:33 AM EAT,
charahani said…
Hudson,
Hongereni sana kwa kupitisha azimio la Dodoma. Nimekuwa nikilisoma kuanzia mwishoni mwa wiki hakika kazi nimeiona na msingi umelala ambao bila shaka juu yake litajengwa hekalu zito la Wanablogu.
Mliyopitisha ni ya msingi sana na yakifuatwa bila shanga tutasonga mbele sana katika ulimwengu huu wa wanablogu
At 2:57 PM EAT,
Innocent said…
Hongereni sana, ninawafuatilia sana.Nitakuja Dodoma mwezi July, hivyo msinisahau.
At 5:36 PM EAT,
Bwaya said…
Mmefanya kazi nzito inayoatahili heshima. Kazi kwetu kulitunza Azimio hili.
At 10:27 AM EAT,
Rashid Mkwinda said…
Azimio la Dodoma nadhani utakuwa ni mwanga kwa wanaBlogu,na iwe basi kwa wanablogu wote kufuata nyayo za wanablogu ha3wa wa Dodoma kwani isije ikawa blogu ikatumika visivyo na wasiopenda amani kwani ipo wazi mno na kila mtu ana uhuru wa kuchangia lolote bila kudhibitiwa na yoyote kwa wakati wowote.
Mie nafikiri kuwepo na Wizara ya nidhamu na maadili kwa wanablog hata kwa wale akina Anonymous waweze kudhibitiwa, wasivuke mipaka, si unajua kuwa mtandao huu unawezaa kukutwa na hata vizazi vyetu vya karne zijazo ilhali sisi tukiwa makaburini isije ikawa kwa vizazi vyetu vikatuona sisi kama wasaliti na kututusi ilhali tumefukiwa ndani ya tani 7 za mchanga kwa miaka zaidi 100 iliyopita
Post a Comment
<< Home